MISSION AND EVANGELISM






CCT YAKABIDHI VITU VYA THAMAN ZAIDI YA MILIONI 50 KWA WAATHIRIKA WA MVUA ZA TOPE HANANG MANYARA

Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT, Baba Askofu Stanley Hotay( Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro) akiambatana na Katibu Mkuu wa CCT Mch.Canon.Dkt Moses Matonya pamoja na baadhi ya Viongozi wa CCT Mikoa na Wilaya wamekabidhi Rasmi Mahitaji muhimu ya waathirika wa mafuriko Kwa uongozi wa Serikali ya wilaya ya Hanang ,Mkoani Manyara. Mahitaji hayo muhimu yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni hamsini (50)vikiwemo simenti,mabati,nguo na vyakula vimekusanywa kupitia CCT mikoa na wadau mbalimbali wa CCT. Akikabidhi mahitaji hayo baba Askofu Stanley Hotay ameishukuru mikoa ya CCT ,wadau mbalimbali na watumishi wa CCT waliotoa mahitaji hayo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko pia amesisitiza uongozi wa Serikali kuhakikisha mahitaji hayo yanawafikia walengwa kwa uaminifu kama ilivyolengwa Akipokea mahitaji hayo Mhe. Janeth Mayanja Mkuu wa Wilaya ya Hanang amewashukuru viongozi wa CCT kwa namna walivoshirikiana na serikali tangu mafuriko yalipotokea ,haswa amewapongeza viongozi wa CCT wilaya ya Hanang kwa namna wanavoshirikiana katika mambo mbalimbali kwenye wilaya hiyo,pia ameahidi vitu vyote vilivyotolewa vitawafikia walengwa kwa uaminifu. Katika hatua nyingine Mhe. Janeth Sanya ameipongeza CCT kwa kuendelea kutekeleza Miradi mbalimbali na kutoa elimu ya saikolojia kwa waathirika wa mafuriko na ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika Miradi na kazi zote za kusaidia jamii zitakazokua zikiendelea wilayani, Hanang.























Katibu Mkuu CCT ashiriki Mkutano wa Wachungaji wote wa KKKT-DODOMA

Katibu Mkuu CCT ashiriki Mkutano wa Wachungaji wote wa KKKT-DODOMA Mkutano wa tano (5) wa Wachungaji wote wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania unaendelea hapa katika ukumbi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Jijini Dodoma. Mkutano ulianza tar 10 Septemba na utahitimishwa tar 15 Septemba 2022, ambapo zaidi ya wachungaji elfu mbili wameweza kusiriki. Katika Mkutano huu Katibu Mkuu wa Jumuitya ya Kikristo Tanzania Mchg. Dkt. Canon Moses Matonya leo tar 13 ametoa pongezi la washiriki kuitikia vizuri mkutano huo. Ambapo pia amewashukuru kwa kuwa KKKT ni Kanisa lenye mchango mkubwa katika kuinarisha umoja wa CCT. Pia amewashukuru kwa kuwa ni moja ya wachungaji wengi wanajitajidi sana kutoa elimu ya kiroho kwa watoto walioko shuleni kupita UKWATA na kwa wanafunzi walioko Vyuoni(USCF). Katibu Mkuu ameeleza kuwa miongini mwa vyanzo vya mapato katika kuimarusha CCT ni sadaka ya CCT Day na michango ya Uanachama, kanisa la KKKT limekuwa mfano mzuri katika kutekeleza hayo. Amewaomba wachungaji kuendelea kuimarisha Upendo wa Yesu Kristo, kwa kuwa tukiwa na Upendo, migogoro kwa Makanisa au familia na sehemu nyingine yoyote haitaweza kutokea. Ametoa wito tuendeleza kuimarisha umoja wetu wa CCT, kwa kuwa tukiwa wamoja tutakuwa na sauti ya pamoja. Ili kuimarisha hili tumeunda uongozi wa CCT Mikoani, hivyo tuutumie uongozi huo katika kuinarisha umoja wetu. Pia amesisitiza washiriki kuzifanya kazi zote kwa pamoja hasa katika kutoa elimu mashuleni na vyuoni ili kila shule au kila darasa liwe na mwalimu wa kiroho. Amehimiza wachungaji kushiriki kikamilifu siku ya CCT Day ili kuimarisha Zaidi chombo hiki. Ujumbe wakati wa Mkutano huu “Lichungeni Kundi la Mungu….” 1Petro 5:2