Mch.Canon.Dkt. Moses Matonya Katibu Mkuu wa Jumuiya Ya Kikristo Tanzania-CCT akiambatana na baadhi ya watumishi wa CCT wametembelea nyumbani kwa Katibu Mkuu Mstaafu wa CCT Askofu Stanford Shauri(1976-1988) Kimara Dar es salaam. Katibu Mkuu Mstaafu wa CCT aliweza kueleza mengi juu ya historia ya CCT ikiwa ni pamoja kuhama kwa makao makuu ya CCT Kutokea Dar es salaam kwenda Dodoma 1970s. Aidha Mtoto wa Katibu Mkuu Mstaafu Mr. Alex Shauri alieleza namna Baba yake alivyoweza kufanya kazi mbalimbali ndani ya CCT ikiwemo usimamizi wa majengo mbalimbali ya CCT likiwemo Jengo la CCT Church House zilipo ofisi za CCT Makao makuu kwa sasa. Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Mstaafu amewashukuru sana viongozi wa CCT Kwa kumtembelea nyumbani kwake huku akikiri kuona upendo wa matendo kutoka ndani ya CCT. Pia ameendelea kuhimiza umoja na mshikamano kati ya makanisa wanachama na vyama vishiriki vya CCT aidha amepongeza kazi kubwa ya uwekezaji wa vitega uchumi inayoendelea kufanywa na CCT