More details

Tamasha la Uimbaji DSM

Tamasha la Uimbaji katika ukumbi wa DPC DSM Leo tar 4 Disemba 2022. Tamasha limeambatana na maombi. Lengo la Tamasha ni kuendelea kuikumbusha jamii kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea kama Ebola ambayo ipo nchi jirani. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo alikuwa Askofu Nelsoni Kisare, ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania. Amesisitiza washiriki kuendelea kujinyenyekeza mbele za Mungu ili kukabiliana na magojwa haya. 2 Nyakati 7:14 Mkurugenzi wa Shirika la Tanzania Interfaith Parrtinership (TIP) Asina Shenduli, ameeleza malengo ya makuu ya kuendesha tamasha hili ambayo ni kuijengea jamii uelewa kupitia uimbaji juu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola na hamasisho la watu kuendelea kupata huduma ya Chanjo ya UVIKO-19.