More details

Kongamano la Maombi na Kampeni ya Kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua Kongamano la Maombi na Kampeni ya Kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia. Katika hotuba yake amepongeza jitihada zinazofanywa na CCT katika kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia Amesema CCT imeunga mkono Serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia. Takwimu Kwa dodoma Kwa mwaka 2021 zinaonesha watu 3696 walifanyiwa ukatili wa kimwili, kingono na hisia. Kwa mwaka 2022 miezi mitatu julai hadi septemba jumla ya watoto 274 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia wengi wao wakiwa watoto wa kike. changamoto ambazo tusaidieane kuzishughulikia ni maadili ya watoto na vijana hata wazazi wenyewe, utoro wa watoto shuleni, ndoa za utotoni. mimba kwa wanafunzi, ufaulu mdogo. Tunatamani kuona watanzania wenye furaha amani na upendo. mtu anayefanyiwa ukatili hawezi kuwa na hayo. Mimi na wewe tunapaswa kusaidiana katika kuielimisha jamii katika kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia. Amewaomba viongozi wa dini kuongeza mafundisho ya maadili katika vipindi vya dini shuleni, na hata katika Makanisa. Kongamano hilo limeandaliwa na Umoja wa Wanawake CCT na kuhudhuriwa na Maaskofu na Wanawake zaidi ya 300 kutoka makanisa 12 wanachama wa CCT toka Mikoa ya Tanzania.