More details

Ibada ya kumwekea mikono Mama askofu Esther Muhagachi kuwa Shemasi wa Kanisa

Ibada ya kumwekea mikono Mama askofu Esther Muhagachi kuwa Shemasi wa Kanisa Tar 22 Jan 2023. Tukio hili limefanyika katika Kanisa la Mennonite Tanzania, Rorya (Shirati) Mkoa wa Mara. Shemasi Esther Muhagachi ni mtumishi wa CCT akisimamia kitengo cha wanawake , watoto na jinsia. Katika tukio hili viongozi wa dini toka makanisa wanachama CCT wameshiriki akiwemo Katibu Mkuu wa CCT Mchg Canon Dkt Moses Matonya. Viongozi wengine walioshiriki ni kutoka Rwanda na Kenya.