More details

Ibada ya siku ya CCT (CCT DAY) Kitaifa Mei 28

Ibada ya Siku ya CCT(CCT DAY ) kitaifa mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro Tar 28 Mei 2023 Katika Kanisa Kuu la KKKT. Ibada ilihudhuriwa na Maaskofu toka Makanisa wanachama CCT na Viongozi wa Vyama shirikishi. Katika ibada hiyo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk Mwigulu Nchemba ambaye alipokea ombi la CCT na kuahidi kushughulikia suala la Kodi zinazotozwa Taasisi za Dini zinapoisaidia SERIKALI kutoa huduma za Afya na Elimu na ununuzi wa vitambaa Kwa wanawake wakati wa hedhi. Amekumbusha pia kwamba maombi hayo yalikwishatolewa maelekezo na Mh. Rais hivyo wakati wa hitimisho la bajeti ya Serikali yatatolewa ufafanuzi.