More details

Ibada ya Mkutano Mkuu wa 56 wa UKWATA Taifa

Ibada ya Mkutano Mkuu wa 56 wa UKWATA Taifa imemalizika Leo Tar 7 Agosti 2022 katika shule ya Martin Luther Jijini Dodoma . Katika mahubiri Askofu Charles Mjema amesisitiza waumini kumjua Mungu na kutembea naye na sio kuishia kumjua tu. Katika ibada hiyo viongozi wapya wa UKWATA Taifa kwa kipindi cha mwaka mmoja(2022/2023) wamechaguliwa, ambapo Raisi wa UKWATA Taifa ni Onesmo wa kulia. Mkutano umeahirishwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania Mchg Can Dkt.Moses Matonya. Neno Isaya 55:8 "....Maana mawazo yangu simawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana..."