More details

SIKU YA MAOMBI YA DUNIA NENO KUU

CCT YAUNGANA NA WAKRISTO WOTE DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA MAOMBI YA DUNIA NENO KUU ‘’Vumilianeni kwa upendo…..’ WAEFESO 4:1-7 Ibada imeandaliwa na kamati ya WDP ya Palestina machi 1, 2024 Ibada inatuita kuvumiliana kwa upendo, licha ya shida na dhuluma zote. Liturujia iliandikwa na kikundi cha wanawake wa Kikristo wa Kipalestina wa kiekumene kwa kuitikia kifungu cha Waefeso 4:1-7. Tulitafakari kwa pamoja mada hii kutoka kwa madaktari wa mateso yetu kama wanawake wa Kikristo wa Palestina. Tunatumaini kuwatia moyo wanawake wengine ulimwenguni kote kuvumiliana kwa upendo wakati wa shida. Picha ni ibada katika kanisa la Anglikana Pareshi ya Mlimwa ambapo wanawake toka Makanisa mbalimbali yaliyoko Dodoma wameshiriki.