More details

Ibada ya kuweka wakfu kiwanja cha Chaplaincy ya CCT katika Chuo Kikuu cha Dodoma

Ibada ya kuweka wakfu kiwanja cha Chaplaincy ya CCT katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) imefanyika leo katika Mtaa wa Nghonghona UDOM ambapo ndipo Kanisa la Chuo Kikuu cha Dodoma litajengwa. Ibada hii imeongozwa na Mratibu wa Chaplaincies za CCT Mchg. David Kalinga mbaye ndie Mkurugenzi wa Utume na Uinjilisti CCT. Ibada hiyo imehudhuriwa na wanafunzi kutoka vitivo vyote katika chuo hicho ambao wako chini ya Makanisa wanchama CCT. Ujenzi wa chaple utaambatana na nyumba kwa ajili ya watumishi wa kuongoza Chaplaincy hiyo. Mwenyeji katika ibada hiyo alikuwa ni Mchg. Timothy Erasto Chimeledya ambaye ndie Chaplain wa UDOM